Nafsi Mbili Ndani Yetu(Yetzer Hara/Yetzer Tov)

  • Bereshit / Mwanzo 1:1-6:8
  • Yeshayahu / Isaya 42:5-43:10
  • Yochanan / Yohana 1:1-14

Bereshit{8:6}Ikawa baada ya siku arubaini kumalizika,Noach alifungua dirisha la safina aliyotengeneza,{8:7}akamtuma kunguru.Akaenda huku na huko,mpaka maji yalipokauka juu ya dunia.{8:8}Akamtuma njiwa kutoka kwake,aende akaangalie kama maji yamekauka juu ya nchi,{8:9}lakini njiwa hakupata mahali pa kukanyaga kwa miguu yake,akarudi kwake katika safina.{8:10}Akakaa kwa muda wa siku saba;kasha akamtuma tena njiwa kutoka katika safina.{8:11}Njiwa akarudi kwake jioni,na,,tazama,katika mdomo wake alikuwa amechukua jani la mzaituni alilochuma.Ndipo Noach alipojua yakuwa maji yamekauka juu ya nchi.{8:12}Akakaa tena siku saba kasha akamtuma tena njiwa;naye hakurudi tena kwake.

Niligundua kitu cha kuvutia sana nilipokuwa nikisoma maandiko yaliyotangulia hapo juu.Tunapo soma kabla ya Noach kumtuma njiwa tunaona ya kwamba alimtuma kunguru. Otaona ya kwamba kunguru hakurudi bali alizunguka huku na huko katika dunia mpaka maji yalipokauka. Kutokana na nijuavyo mimi kutokana na yale yaliyoandikwa, kunguru anaweza kuwa alizunguka kwa muda wa siku saba kwa uchache sana bila kutua popote wala bila kula chochote.

Kunguguru ni ndege walio najisi kwa hiyo walikuwa wawili tu katika safina; Noach alimtuma mmoja . Ili waweze kuzaana ilikuwa lazima ndege hawa waweze kukutana tena mmoja na ule mwingine aliyesalia katika safina. Je, kunguru anaweza kupaa akizunguka huku na huko kwa siku saba bila kula chochote wala kutua popote?Hapana, isingewezekana. Hata viyo kunguru kama nilivyosema, kunguru ni ndege asiye safi isitoshe, ni ndege alaye mizoga. Ikiwa ni hivyo basi, lazima angelipata chakula. Na zaidi ya hayo , kunguru lazima angelipata mahali pakutua katika mizoga iliyotapakaa kote, mizoga ya wanyama na mizoga ya watu iliyokuwa ikielea juu ya maji pande zote huku ikiwa ime fura na kupasuka. Kwa hiyo hakuhitaji kurudi katika safina.

Njiwa kwa upande mwingine, ni ndege walio safi. Hawali mizoga. Kwa hivyo njiwa aliyetumwa na Naoach asingeliweza kupata chakula. Hakukuwa na chakula wala mahala pa kutua ilimlazimu njiwa yule kurudi katika safina.

Kuna funzo kubwa sana la kiroho hapa. Kumbuka ya kwamba, kulikuwako na wanyama najisi na wa sio najisi katika safina, na wote wali kuwa mahali pamoja. Pia kumbuka ya kwamba, HaShem ( Mungu) ameugawanya ulimwngu katika matabaka mawili ama maumbile ya aina mbili, ama uasili wa aina mbili, najisi na safi. Lakini lakuhuzunisha ni kwamba sisi kama watu wanaomwamini Yeshua HaMashiach tuna asili hizi mbili ndani yetu.

Romim { 7:18} Najua ya kwamba hakuna kilicho kizuri ndani yangu,yaani katika mwili wangu : Napenda kufanya vizuri lakini uwezo wa kufanya lililo jema sina.

Shaul ( Paulo) alikuwa akielezea hali ya uasili wetu unavyovutana mmoja na mwingine. Kuna mashindano yanayo endelea ndani yetu. Mapambano yenyewe ni kati ya mtu wa kale( Mwili) na mtu mpya( mtu aliye zaliwa upya katika roho). Yule kunguru aliyetumwa kwenda katika ulimwengu alikuwa amejaa kifo na mauti lakini kwake ilikiwa ni sherehe. Ali ruka huku na huko katika dunia akidonadona mizoga ya walio kufa. Hi ni hali ya uasili wetu wakale. Huyo mtu wa kale anapenda mambo ya ulimwengu na anayafurahia na kuyasherehekea. Lakini yale ulimwengu unayopatiana ni mauti. Njiwa kwa upande mwingine ana wakilisha utu upya ( Mtu mpya). Hakuona chochote katika ulimwengu ambacho juu yake angekita miguu yake, haku wona chochote killicho mtia hamu ya kukila, kwa hiyo ilimbidi arudi kutafuta hifadhi na usalama katika safina ( Yeshua HaMashiach).

Kama waaminio, tuko katika ulimwengu lakini sisi si wa ulimwenguni. Hatupaswi kurithishwa na chochote cha ulimwengu. Ulimwengu unatuhitaji sisi zaidi kuliko sisi tunavyo uhitaji; kwa hiyo tuna paswa kuutumia ulimwengu kama jukwaa la kuwavuta waliopotea ( ambao hawajaokoka) kwa Yeshua HaMashiach, kutoka ulemwnegu ya uwongo na kuwaelekeza katika kweli.

Kwa kunguru mauti na ulimwengu uliokufa ulimvutia; alitaka kuishi akishikamana na ulimwengu ule. Lakini njiwa aliweza kutambua ya kwamba hakukuwa na chochote katika ulimwengu. Aliweza kupata pumziko lake katika safina.

Wewe mwenyewe wajihusisha na ndege yupi kati ya hawa wawili katika maisha yako?

facebooktwittergoogle_plusredditpinterestlinkedintumblrmail