Kutuvika Na Haki Yake

  • Vayikra / Walawi 6:1-8:36
  • Malachi / Malaki 3:4-24
  • Wayahudi Wamasihi / Waebrania 8:1-6

Vayikra{8:1}HaShem akanena na Moshe nakusema,{8:2}Mchukue aharon na wanawe pamoja naye,na mavazi,na mafuta ya kuweka wakfu,na fahali wa sadaka ya dhambi,na kondoo wawili,na kapu la matzah(mkate usio tiwa chachu);{8:3},na ukusanye kehilah(kusanyiko yote katika lango la Ohel Moed(hema ya kukutania).{18:4}Moshe akafanya kama HaShem alivyomwamuru;na watu walikuwa wamekusanyika katika lango la Ohel Moed.{8:5}Moshe akaliambia kusanyiko,hili ndilo jambo ambalo HaShem ameamuru litendwe.{8:6}Moshe akawaleta Aharon na wanawe na kuwaogesha kwa maji.{8:7}Akamvika Aharon vazi na nguo ya utmishi ndefu na akamvika efodi juu yake na akamfunga kwa mkanda ulioundwa kwa ustadi wa efodi.{8:8} Akamvika darii na katika darii akaweka Urim na Thummim.{8:9}Akamweka kilemba kichwani,upande wake wa mbele akaweka kijisahani cha dhahabu,taji kadosh(takatifu);kama HaShem alivyomwamuru Moshe.

Nimeonesha sehemu ndogo tu ya yale ambayo HaShem alimwamuru Moshe kuwafanyia Aharon pamoja na wanawe,alipokuwa akiwaweka wakfu kwa ajili ya utumishi wake HaShem.Inanishangaza ni kwanini HaShem alimfanya Moshe afanye mambo haya aina mbalimabali kwa Aharon na wanawe.Ni dhahiri wangaliweza kuoga wenyewe(huku hakukuwa kuoga kwa kawaida,ilikuwa ni ,kuzikwa majini,pia wangaliweza kujivika mavazi wenyewe na kufanya mambo mengine ya lazima ili kujitolea sadaka wao wenyewe kama vile ambavyo wangalifanya siku za mbeleni.Kwanini basi,HaShem alimwamuru Moshe kuwaogesha na kuwavika?

Naamini jibu ni dhahiri.Aliye mkuu ndiye anayemfanyia uteuzi aliye mdogo nadhani sote twafahamu hilo.tulipokuwa tunafuzu shuleni,bila kujali ni daraja gain,ilikuwa ni msimamizi wa shule,au msimamizi wa kitengo husika,aliyepewa hadhi ya kuendesha sherehe za kufuzu na ili kutuvukisha daraja na sio sisi wenyewe.Kwahivyo inaeleweka kuwa Moshe aliye mkuu angaliwaweka wakfu walio wa chini yake-Aharon na wanawe.

Shemot(kutoka){33:11} HaShem alinena na Moshe uso kwa uso,kama vile ish anenavyo na rafikiye.

Bamidbar{12:6}Akasema,Sikiliza sasa maneno yangu:kama kuna navii kati yenu,Mimi HaShem nitajifunua kwa mtu huyo katika maono,nitanena na mtu huyo kupitia ndoto.{12:7}Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Moshe;Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote:{12:}yeye nanena naye mdomo kwa mdomo,wazi wazi,na wala si kwa mafumbo;na umbo la HaShem ataliona:kwanini basi nyinyi hamkuogopa kunena dhidi ya mtumishi wangu,dhidi ya Moshe?

Moshe hakuwa mtu wa kawaida.HaShem alimweka wakfu na hili ni dhahiri katika mafungu yaliyotangulia hapo juu,HaShem alimfanya kuwa mtu wa kipekee.Kwa uhakika,HaShem alimfanya kuwa mfano wa Yeshua HaMashiach.Tukiyazingatia hayo,hebu tuangalie ni nini Moshe alifanya kwa makuhani na kwa ukuhani kwa ujumla,na tufananishe na yale ambayo Yeshua katutendea sisi.

Yeshua HaMashiach ametuosha sisi,ametufanya safi kupitia Neno Lake na Damu yake.Alijitoa mwenyewe ili kuwa Kapparah yetu(upatanisho).Alituvua mavazi ya kale yaliyokuwa yamegandama dhambi na akatuvika mavazi mapya ya ukuhani yaliyostahili kuturuhusu kukiendea kiti cha enzi cha Mungu.Kwa kutuvika haki yake Yeshua ametufanya kuwa haki-Mkuu kamteua aliye chini yake.

Moshe aliwavika Aharon na wanawe mavazi ya haki ya ukuhani.Kutokana na aina ya vitu vilivyotumika,vitu tofauti tofauti,pamoja na rangi,na vitu vilivyotengeneza vitu hivyo,vilisimamia kuvaa haki ya Yeshua HaMashiach.Sura bora kabisa ya yale Yeshua aliyotutendea.

facebooktwittergoogle_plusredditpinterestlinkedintumblrmail