Baada ya kifo-watakatifu

  • Vayikra / Walawi 16:1-20-27
  • Amos/Amosi 9:7-15
  • Korintim Alef/1 Wakontho 6:9-20
  • Mattityahu/Mathayo 5:43-48

Vayikra{16:3} Kutokea hapo Aharon atakuja na kuingia Kadosh Kedoshim (Patakatifu Pa Patakatifu) pamoja na fahali kama sadaka ya dhambi na ndume wa kondoo kama (olah) sadaka ya kuteketeza.{16:4} Atavaa koti kadosh (takatifu) ya kitani naye atakuwa na vazi la kitani la ndani juu ya mwili wake,na atajifunga kwa mshipi wa kitani na kwa kofia maalum atavikwa:haya ni mavazi matakatifu;naye atauogesha mwili wake katika maji na kuyavaa mavazi yale.Vayikra{[16:23} Aharon halafu atakuja katika Ohel Moed (hema ya kukutania),na atayatoa mavazi yale ya kitani,ambayo aliyavaa alipoingia Kadosh Kedoshim (Patakatifu Pa Patakatifu),na kuyaacha hapo:{16:24} na atauzamisha mwili wake katika maji mahali patakatifu,na kuvaa mavazi yake,na kuja na kutoa olah korban ya watu(sadaka ya kuteketeza) na kufanya Kapparah(upatanisho) kati yake na watu.

Yaliyonivutia katika parashot (sehemu hizi mbili za Torah) katika Masomo yetu ya juma hili,ni ya kwamba yanahusiana na mavazi.Katika fungu letu la kwanza tulilo soma hapo juu,tunaona ilimbidi Aharon abadili mavazi aliyokuwa amevaa alipoingia Kadosh Kedoshim.HaShem alimtaka avue mavazi ya kikuhani na kuvaa vazi la kitani,nguo ya nje na ndani mshipi na namna ya kofia kichwani mwake.Hili ni jambo la kuvutia kwasababu ni HaShem mwenyewe aliyebuni na kumfanya Aharon avae kilichobuniwa na kufanywa kwa ustadi,kurembwa kwa mchanganyiko wa rangi na kufumwa kiufundi,uzi safi na nguo ya kitani.Hata tumepewa sababu ya mavazi yale Aharon aliyotakikana kuyavaa:

Shemot(kutoka) {28:2} Na utamfanyia Aharon kaka yako mavazi matakatifu,kwa utukufu na maridadi.Yalikuwa ni kwa urembo na utukufu alipoyavaa na kuja mbele ya bnei Yisrael(wana wa Yisrael).Ingawaje tunajulishwa kuwa hata kama Aharon angaliweza kuvaa mavazi yale mbele ya bnei Yisrael,lazima angaliyavua,kuvaa mvazi mengine yaliyo ya kitani safi nyeupe alipokuwa anakwenda mbele za HaShem nyuma ya pazia.Utaona kwamba,baada ya kumaliza shughuli alizotakikana kufanya mbele ya HaShem,ilimpas kuyavua mavazi yale ya kitani,kuyaacha mahali patakatifu na kuvaa mavazi rasmi ya Kohen HaGadol.Alikatazwa kabisa kutovaa mavazi ya kitani hadharani.Alipokuwa akihudumu hadharani,ilimpasa kuvaa mvazi yake rasmi ya ukuhani yaliyorembwa katika utimilifu wake kama Cohen HaGadol.

Sababu moja tunayopewa ya kuvaa kitani ni jasho,kama ilivyo katika Yechezkiel(Ezekieli) 44:15.Hata hivyo,ninapendekeza sababu nyingine,ile ambayo,hata kama haijatajwa wazi wazi kwenye Maandiko kuhusu kuingia katika Kadosh Kedoshim,imetajwa kwingi katika Maandiko,na ni hili:

Iyov(Ayubu){38:4}”Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?Niambie kama unaufahamu,{38:5} Ni nani aliyefanya vipimo vyake,kwa kuwa wajidai wajua? Ama ni nani aliyefanya mstari juu yake?

Cohen HaGadol alimwakilisha HaShem kwa watu;kwa hivyo,kabla ya kwenda mbele za HaShem alimtaka awe amevaa mavazi ya rangi nzuri na yaliyorembeka sawa sawa na Yule yaliyokusudiwa kumuwakilisha.Kutokana na huduma yake na Yule aliyemwakilisha,Cohen HaGadol alikuwa wa kuogopwa na kupewa heshima na hadhi.Lakini alipokwenda mbele za HaShem,aliwawakilisha watu mbele zake na Maandiko tuliyoyanukuu hapo juu ya Iyov yadhihirishavyo,mwanadamu kujiona jinsi alivyo hasa inapomuhusisha HaShem.

Hata hivi leo,kama viongozi wa kiroho na washirika,lazima tuwe na mtazamo ulio bora na hai,tupokwenda mbele za HaShem katika maombi na kuabudu.Viongozi wa kiroho kulingana na nafasi zao,wanamwakilisha HaShem kwa watu;kwa hivyo,ni lazima wawe watu wasio lawama hadharani na katika maisha yao ya kibinafsi na kwasbabu ya nafasi zile wanazoshikilia,wapewe heshima.Hata hivyo,viongozi hawa wakiroho,wanapowakilisha kusanyiko mbele za HaShem katika kuomba na kuabudu,lazima wafanye hivyo kwa unyenyekevu na moyo uliopondeka.

Kulingana na nafasi zao,viongozi wa kisiasa wanastahili heshima,ila kwa kuhusiana na HaShem,wanapaswa kuwa wanyenyekevu.Hili si chaguo la mtu kama apendavyo,hili ni agizo la kibiblia.

facebooktwittergoogle_plusredditpinterestlinkedintumblrmail