Categorized: 5766, Haazinu-ks, Kiswahili, Sefer Devarim (Deuteronomy), Torah Portion
Hakuna Kipya Katika ‘agano’ Jipya!

Hakuna Kipya Katika ‘agano’ Jipya!

  • Devarim / Kumbukumbu ya Torati 32:1-52
  • Hoshea / Hosea 14:2-10
  • Yo’el / Yoeli 2:11-27
  • Mikhah / Mika 7:18-20
  • Romim / Warumi 10:14-11:12

Katika Parasha ya wiki hii Moshe anaimba nyimbo nzito kuhusu upeo wa mbeleni wa bnei Yisraeli (wana wa Israeli). Maneno yake yanatoa unabii juu ya shingo zao ngumu na mioyo yao migumu, ambayo hatimaye itawafanya wao kuanguka katika ibada ya sanamu na mwishowe itawagharimu vibaya. Mashairi yake yanaelezea kwamba Yisraeli itasambaratika na kutawanywa kati ya mataifa, yote ni kwa sababu wamemgeuzia M-ngu wao migongo yao, ambayo itaashiria Yeye kuugeuzia mgongo Wake kwao.

Katika usomaji wa mistari ya nyimbo hii ningalipenda tujifunze kuelewa madhara ya dhambi. Wengi wetu tunaamini kwamba dhambi zetu siyo ibada ya sanamu. Ingawa zinaweza kuonekana kwetu hazina madhara au siyo za maana sana, kam vile kusema uongo mdogo usio na madhara au kuchukua stampu ya posta ofisini kwetu bila ya kibali, bado zinabakia kuwa ni ibada ya sanamu. Unaweza kujaribu kujiburai wewe mwenyewe kwa kusema kwamba unamwamini M-ngu na hata iwapo wewe si mwanadamu mkamilifu lakini huabudu sanamu yoyote. Pole sana, maana nina habari za kusikitisha kwako! Kila dhambi, haijalishi ni ndogo kiasi gani au ni hafifu kiasi gani, bado ni dhambi machoni pa M-ngu, na dhambi yote ni ibada ya sanamu kiasili. Je, inawezekanaje iwe hivyo? Ni rahisi sana! Dhambi yako inakataaa na kupinga mamlaka ya M-ngu, kwahiyo; unajiweka mwenyewe, mahitaji yako, tamaa zako, juu ya M-ngu na hilo ni ibada ya sanamu!

Baada ya kukushirikisha wewe hili, hapa ni kifungu kutoka Parasha hii ambacho kimenitakabahi na ambacho ningalipenda kukitolea hoja:

Devarim / Kumbukumbu{32:39} Oneni kuwa mimi ndimi M-NGU na wala hakuna mwingine ila Mimi. Mimi huua na kuweka hai; hujeruhi na kuponya, na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi Mwangu. {32:40}Kwani nainua mkono wangu mbinguni, na nasema, kama niishivyo milele, {32:41}Kama nikiunoa upanga Wangu umeremetao, mkono Wangu ukashika mishpat(hukumu); Nitawalipiza kisasi maadui Wangu, Nitawaadhibu wale wanaonichukiao. {32:42}Mishale Yangu nitailevya kwa damu, upanga wangu utashiba nyama, utaloana damu ya waliochinjwa na mateka, kuanzia kichwa cha viongozi wa adui.” {32:43}Enyi mataifa shangilieni, [pamoja] na watu Wake: maana Atailipizia kisasi damu ya watumishi Wake, Atalipiza kisasi kwa wapinzani Wake, Atatoa upatanisho kwa ajili ya nchi Yake na watu Wake.

Mara nyingi tunasikia kauli kama “Naapa mbele za M-ngu.” Na labda hata wewe mwenyewe umeshawahi kujisemea hivyo. Uzoefu huu wa kuapa kumtumia M-ngu kama shahidi hutumika kama njia ya kuhalalisha ukweli na unyofu wa kile kinachosemwa. Sikubaliani na uzoefu huu wa kuapa kwa kutumia jina la M-ngu. Kwanza, neno la mtu lazima liwe katika shahada yake, hasa kwa yule amwaminie Yeshua HaMashiakhi, Maana Yeshua HaMashiakhi alisema:

Mattityahu (Mathayo) {5:37} “Basi, na matamshi yawe, ‘Ndiyo, ndiyo’ {au} ‘Hapana, hapana’; na chochote kinachozidi hayo hutoka kwa mwovu.

Ingawa inatakiwa tusiape kwa kutumia jina la M-ngu au kitu kingine chochote, katika jambo hilo hapa katika Parasha Ha’azinu tunaona M-ngu akiapa kwa jina Lake Mwenyewe. Je, Biblia inajipinga yenyewe? Hapana, M-ngu anaruhusiwa kuapa kwa jina Lake Mwenyewe, kwanza ni kwa sababu hakuna aliye mkuu kuliko Yeye wa kuapiwa, na pili ni kwamba hakuna uwezekano wowote wa kwamba lile Analolisema ni uongo. Ukweli siyo kwamba M-ngu akijiapia kwa jina lake Mwenyewe ndiyo jambo linivutialo, bali hasa kile M-ngu anachoapa ndicho kimenifanya niwe makini.

Mwanzo wa Parasha yetu HaShem anawaambia Yisraeli juu ya mambo yote ya kutisha ambayo yatawaangukia kutokana na ibada zao za sanamu. Katika jambo moja, tunaweza kuona kutokana na mistari hii, kwamba mataifa mengine yatawakandamiza.

Devarim {32:22}Hasira Yangu imewaka moto, inachoma mpaka chini kuzimu, itateketeza dunia na vilivyomo, itaunguza misingi ya milima. {32:23} Nitarundika maafa chungu nzima juu yao. Nitawamalizia mishale yangu: {32:24} Watakonda kwa njaa, na wataangamizwa na joto lichomayo na uharibifu mchungu, Nitapeleka wanyama wenye meno makali kuwashambulia, pamoja na vitu vyenye sumu vitambaavyo mavumbini. {32:25}Vita vitasababisha vifo vingi nje na majumbani hofu itawatawala, wote vijana ish(wanaume) na bikira, wanyonyao pamoja na ish wenye mvi. {32:26}Nilisema, Ningaliwasambaratisha mbali, nitawafanya wasikumbukwe tena kati ya watu;”

Lakini mwisho wa Parasha hii, HaShem anaahidi, kwa kujiapia Mwenyewe kujilipizia kisasi kwa ajili ya watu Wake, kwa kiasi ambacho mataifa yaliyo wakandamiza sasa yatawashangilia watu Wake. Kumbuka yale HaShem aliyasema katika Devarim 32:43:

Devarim {32:43} Enyi mataifa shangilieni, [pamoja] na watu Wake: maana Atailipizia kisasi damu ya watumishi Wake, Atalipiza kisasi kwa wapinzani Wake, Atatoa upatanisho kwa ajili ya nchi Yake na watu Wake.

Moshe anatoa mada nne hapa ambazo zinafungamana na Kitabu cha Hitgalut (Ufunuo) na ujio wa Enzi za Kimasihi. Naamini hakika kwamba kile Moshe anakiongelea hapa ni nyakati ya mwisho, yaani wakati Yeshua HaMashiakhi atakaporudi baada ya muda wa dhiki, wakati wa adha ya Ya’akov (Yakobo), na kujilipizia kisasi juu ya maadui wa Yisraeli.

Kwa kusema vile kwamba mataifa watashangilia pamoja na watu Wake, HaShem anatuachia sisi tujue kwamba, si tu Yisraeli wataokolewa katika siku za mwisho, bali pia na wengi kutoka katika mataifa ya ulimwengu, na ndiyo watakaokuwa wanashangilia katika BWANA. HaShem anasema vilevile kwamba Atawaangamiza maadui wa Yisraeli, na tunajua kutoka katika Hitgalut kwamba jambo hili litafanyika katika mapambano ya Armageddoni. Mwisho HaShem anasema ataifidia nchi ya Yisraeli katika swala la mafanikio na Atawarudisha nyumbani watu Wake Aliowatawanyisha.

Hapa kwahiyo ni thibitisho moja zaidi ya lile nimekuwa daima nakisema; “Hakuna Kipya Katika ‘Agano’ Jipya!” Kile Yokhanani (Yohana) alikiandika katika Higalut ni kile ambacho tayari Moshe alikitolea unabii katika Devarim miaka maelfu ya mwanzoni.

Enjoyed this Post? Subscribe to our RSS Feed, Follow us on Twitter, make a Comment or simply recommend us to friends and colleagues!

Tzedakah

More Related Articles:


Leave a Reply

Parashat Balak / פרשת בלק
Torah Portion: Numbers 19:1-22:1


  1. Bamidbar 22:2-12 (Sunday)
  2. Bamidbar 22:13-20 (Monday)
  3. Bamidbar 22:21-38 (Tuesday)
  4. Bamidbar 22:39-23:12 (Wednesday)
  5. Bamidbar 23:13-26 (Thursday)
  6. Bamidbar 23:27-24:13 (Friday)
  7. Bamidbar 24:14-25:9 (Saturday)

Haftarah / Prophets

  • Micah 5:6 - 6:8 (Saturday)

Besorah / Good News

  • 1 Corinthians 1:20-31 (Saturday)
Radio Mashiach
Sifrei Chaim - Messianic Jewish Judaica
Tzedakah
Find out on Facebook

Important Links

Special links

  • Offering New Alternatives to Homosexuality
Contact us

A Torah centred Messianic Jewish יהודים משיחים kehila, Toronto, Ontario, Canada - An ever changing Messianic Jewish website till King Mashiach Yeshua comes back!!!
אנחנו רוצים משיח עכשיו / Мы хотим Машиаха сейчас / We Want Mashiach Now / Queremos al Mashiaj ya - יחי אדוננו מורנו ורבינו מלך המשיח לעולם ועד