- Devarim / Kumbukumbu Ya Torati 1:1-3:22
- Yeshayahu / Isaya 1:1-27
- Timoteos Aleph / 1 Timotheo 3:1-7
Devarim {2:4} Waamuruni watu, mkisema, Mko karibu kupita mipakani katika nchi ya milima ya Seiri, nchi ya ndugu zenu bnei (wazawa wa) Esavu (Esau); nao watawaogopeni: lakini mwe na tahadhari; {2:5} msipigane nao; kwa sababu sitawapeni hata mahali padogo pa kukanyaga; Nchi hiyo ya Har (Milima ya) Seiri nimewapa wazawa wa Esavu iwe mali yao. .
Devarim {2:18} "Leo hii mtavuka mpaka Moavu (Moabu) kwa kupitia nchi ya Ari: {2:19} na mtakapoifikia nchi ya bnei Amoni. Msiwasumbue wala msipigane nao kwa kuwa sitawapeni sehemu yoyote ya hao bnei Amoni; iwe mali yenu. La! Hao ni wazawa wa Loti, na nimewapa hiyo nchi iwe mali yao.’"
Devarim {2:24} Kisha HaShem alituamuru: ‘Haya! Anzeni safari. vukeni bonde la Arnoni. Mimi nimeitia mikononi mwenu Sihoni, mfalme wa Waamori wa Heshboni na nchi yake. Mshambulieni na kuanza kuimiliki nchi yake. {2:25} Leo Nitaanza kuwafanya watu wote duniani wawe na woga na hofu juu yenu; watasikia habari zenu nao watatetemeka na kufadhaika.’
Devarim {3:1} Kisha, tuligeuka, tukapanda kuelekea Bashani. Mfalme Ogu alitoka na watu wake wote kupigana nasi karibu na mji wa Edrei. {3:2} lakini HaShem aliniambia, ‘Usimwogope, maana nimemtia mikononi mwako pamoja na watu wake na nchi yake. Utamtendea kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori aliyekaa kule Heshboni’.
Je, umesoma visehemu vinne vya Andiko nilivyovitoa? Utahitaji kufanya hivyo kama unataka kweli kuelewa kile nachotaka kuongelea kuhusu Parasha ya Devarim.
Kutokana na Maandiko haya nimepata kuelewa kwamba kuna baadhi ya mapambano ambayo HaShem hakutaka bnei Yisraeli wayapiganie. Kama wangeachwa wao wenyewe labda wangeshambulia na kuzipiga vita kila nchi zilizowapinga. Kama wangalifanya hivyo, hakika kuna baadhi ya mapambano ambayo wangali yapoteza. Hii bila shaka kabisa ingalitokana na sababu ya kwamba HaShem hakutaka wapigane nao katika jambo hilo hilo. Vile vile naamini kuna mapambano ambayo HaShem hataki sisi tuyapiganie.
Filosofia yangu ambayo nimeishawahi kukushirikisha huko nyuma ni hii, kama unataka kujua jinsi M-ngu anakutendea katika maisha yako, basi, jifunze katika Maandiko jinsi Alivyowatendea bnei Yisraeli. Waweza kujifunza mengi kutokana na jinsi HaShem alivyowatendea wana Wake, bnei Yisraeli, kupitia historia nzima, maana hivyo ndivyo Anavyotutendea sisi wana Wake!
Waweza kuona kile ninachoenda kukuelezea ni cha upuuzi kidogo, lakini naamini kwamba kile nachoenda kuelezea kimehakikishwa na Neno la M-ngu kama ilivyo katika visehemu ulivyosoma hapo juu.
Ninapo wapa ushauri nasaa watu waliochumbiana, hata watu waliooana katika jambo hilo hilo, nawaambia (zaidi wanaume) kwamba wanahitaji kuchagua ni kitu gani hasa cha kupigania. Nawahimiza wasibishane na wenzi wao juu ya kila kipegele, bali wachague kwa makini sana ni kitu gani hasa wagombanie. Sio kila pambano linahitajika kulipigania na kuna mapigano ambayo inatubidi tujiepushe nayo ili kwamba tuishi kupambana na yale makubwa. Kama mume na mke watachagua kupigania kila kitu kinachowakera, basi magomvi hayataisha na hakutakuwa na amani nyumbani. Kuongezea hapo, kupigania kila kitu kunaleta picha ya kwamba kila mara unataka uwe na njia zako mwenyewe, kitu ambacho kinaongeza msuguano katika familia. Wanaume hatutakiwi tuwe waonevu ambao tunalazimisha njia zetu juu ya wake zetu na familia zetu na tabia za kikatili, lakini kuna mambo mengine wakati inakuja katika kuendesha misingi ya kibiblia katika familia, hapo tunatakiwa tuchukue msimamo mgumu juu yake. Ni mapambano ya aina hii inatubidi tuwekee mapigano yetu.
Ni katika hatua hii yao ya kihistoria bnei Yisraeli walikuwa na uhusiano mzuri sana na M-ngu wao, na walipomtaka ushauri Wake, Aliwaongoza siyo tu katika mapambano gani wayapiganie, lakini pia katika vipengele vyote vya maisha yao. Aina hii ya uongozi na muongozo kutoka kwa M-ngu ipo kwa ajili yetu pia kama tunamweka M-ngu katikati ya ndoa zetu na maisha yetu, na iwapo wewe hujaoa au kuolewa, akiwa katikati ya maisha yako pia. Siyo mapambano yote yanayojiweka mbele yako yanamaanisha yapiganiwe na siyo maadui wote wanaokujia kukupinga wanamaanisha uwashinde. Walakini kama ukimuhusisha M-ngu katika kila kitu katika maisha yako, Atakuongoza katika njia yako.
Mishlei (Mithali) {3:6} Umtambue M-ngu katika kila ufanyalo, Naye atazinyosha njia zako.
Enjoyed this Post? Subscribe to our RSS Feed, Follow us on Twitter, make a Comment or simply recommend us to friends and colleagues!

Bookmark

Write to us








