BaMidbar/Hesabu 8:1-12:16 Zecharya/Zakaria 2:14-4:7 Korintim Alef/1Wakorintho 10:6-13 Bamidbar{8:9} Utawaleta Leviim(Walawi) mbele ya Ohel Moed(Heme ya kukutania):na utakusanya kehilah (kusanyiko) yote ya bnei Yisrael(wana wa Yisrael):{8:10} nawe utawaonyesha Leviim mbele za HaShem.Bnei Yisrael wataweka mikono yao juu ya Leviim:{8:11} na Aharon atawatoa Leviim kama sadaka mbele za HaShem kama sadaka ya kutikisa kwa niaba ya bnei [...]









