Shemot / Kutoka 27:20-30:10 Yechezkiel/Ezekiel 43:10-27 Ivrim/WaEbrania 13:10-17 Shemot{28:1}”Mlete Aharon(Haruni) kaka yako,na wanawe pamoja naye,karabu nawe,mbali na bnei Yisrael(wana wa Yisrael,ili anihudumie Mimi katika huduma ya ukuhani,huyo Aharon,Nadav na Avihu,El’azar na Ithamar,wana wa Aharon.{28:2}Utafanya kadosh(takatifu) mavazi ya Aharon kaka yako,kwa kavod(utukufu) na kwa maridadi.{28:3} Utawanenea wote walio na moyo wa hekima,ambao nimewajaza na roho wa [...]









