Categorized: 5769, Kiswahili, Sefer Shemot (Exodus), Torah Portion, Yitro-ks
Uangaliaji Wa Kile Kitakachotokea

Uangaliaji Wa Kile Kitakachotokea

  • Shemot / Kutoka 18:1-20:23
  • Yeshayahu / Isaya 6:1-7:6; 9:5-6
  • Mattityahu / Mathayo 5:5-20

Shemot {19:10} Naye HaShem akamwambia Moshe (Mose), “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu leo na kesho. Waambie wafue nguo zao, {19:11} na wawe tayari katika siku ya tatu, kwa sababu siku hiyo, HaShem atashuka juu ya Hari (Mlima) Sinai machoni pa watu wote. {19:12} Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu uwaambie, ‘Mwe waangalifu msije mkapanda mlimani, au kuugusa. Ye yote atakayeugusa mlima hakika atauawa. {19:13} Hakika atapigwa mawe au kupigwa mishale, mkono wa mtu hautamgusa. Akiwa mwanadamu au mnyama, hataruhusiwa kuishi.’ Ila tu wakati shofari itakapopigwa kwa mfululizo, ndipo watu wote watakapopanda mlimani.’"

Kama ulikuwapo katika ibada yetu ya Shabbati ya wiki ya tarehe 28 Tevet 5769 (Januari 25, 2009), basi, ulikuwa umebarikiwa. Maana siyo tu ibada ilikuwa ina upako, bali pia ulisikia maelezo bora juu ya somo kuhusu wito wa M-gu kwa Yisraeli (Israeli) katika nchi ya ahadi. Pamoja na maelezo haya kulikuwapo na somo juu ya mada egemezo kuhusiana na Hari (Mlima) Sinai katika mpango wa M-ngu kwa Yisraeli.

Katika Parasha yetu ya wiki, Parasha Yitro, hasa kifungu nilichonukuu hapo juu, tunaona HaShem akiwaita bnei Yisraeli kuja karibu na Hari Sinai. Je, hii ina maana gani kuja karibu na Hari Sinai? Ni kipi cha umuhimu sana kuhusiana na Hari Sinai hata kwamba HaShem anawaita watu Wake kuusogelea?

Kuna “namna” nyingi katika Andiko. Tumemaliza tu kujifunza kuhusiana na Yosefu, mwana wa Ya’akovu (Yakobo), ambaye tulimwona kuwa ni namna ya Yeshua. Katika somo letu la Torati la asubuhi ya Shabbati, wiki mbili zilizopita, tuliwaona pia ndugu zake Yosefu waliosababisha auzwe utumwani, walikuwa ni namna ya Yuda Iskarioti aliyemuuza Yeshua. Basi, hapa katika kisehemu cha Andiko kilichonukuliwa hapo juu, naona Hari Sinai kuwa ni namna ya kile kitakachotokea katika enzi ya milleniam (kipindi cha miaka elfu moja), na hii ndiyo sababu ya hoja yangu:

Katika Kitabu cha Yekhezikieli (Ezekieli) tunaambiwa:

Yekhezikieli {47:1} Yule mtu akanirudisha mpaka kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki.) Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kulia mwa Hekalu, kusini mwa Mitsibeakhi (Madhabahu ya Dhabihu za Kuteketezwa).

Katika kisehemu hiki cha Andiko Yekhezikieli analielezea Hekalu la milleniam, ambalo litakaliwa na Mashiakhi (Masihi) wetu arejeapo tena. Yekhezikieli anatumia taswira ya maji yanayo tiririka chini ya kinzingiti cha Hekalu kuelezea Neno la M-ngu likienenda toka Yerushalyim (Yerusalem). Kama tusomavyo katika kifungu hiki cha unabii wa Yekhezikieli tunaona maji haya yakileta uponyaji na uhai kwa kila kitu yakigusacho. Kwa Yekhezikieli inaeleweka kwamba, maji haya ni Neno la M-ngu, yaani Torati, maana hakukuwa na Neno lingine tena wakati ule.

Tena katika Kitabu cha Hitigaluti (Ufunuo) tunaambiwa yafuatayo:

Hitigaluti {22:1} Kisha yule malaika akanionyesha mto wa Maji ya Uhai, maangavu kama kioo yakitiririka kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo,

Maji haya ya Uhai tunayoambiwa katika Andiko hili pia, ni Neno la M-ngu ambalo litaenenda toka katika kiti cha enzi cha HaShem na Yeshua (Mwana Kondoo). Wakati Yokhanani (Yohana) aliandika Hitigaluti, ingawa hii nyaraka ya kitume inaweza kuwa ilikuwa katika mzunguko wakati ule, bado hazikuwa ni sehemu ya kanuni ya kibiblia (yaani vitabu vya Biblia ambavyo vimeunganishwa pamoja kuifanya Biblia iwe kama tuijuavyo sasa) ; bali zilikuwa ni nyaraka tu. Hivyo, Maji ya Uhai, ambayo ni Neno la M-ngu, yangemaanisha Torati ya M-ngu kwa Yokhanani.

Kwa hiyo kile tunachokiona hapa katika visehemu hivi vyote, vinaelezea Neno la M-ngu likienezwa kutoka kwa M-ngu na kwenda ulimwenguni kote. Kisehemu kimoja, kisehemu kile cha Yekhezikieli kinaelezea nyakati za milleniam wakati Yeshua atakaporudi kutwaa Hekalu la Milleniam. Kisehemu kingine, kile cha Hitigaluti, kinaelezea nyakati za mwisho wakati Neno la M-ngu litaenenda toka kwa wote Baba na Mwana kutoka katika Hekalu la mbinguni. Hivyo, ingawa matukio yote yako katika nyakati tofauti, bado yote yanaelezea matukio yafananayo.

Sasa, kama nilivyosema hapo awali, angalia tena Parasha ya wiki hii, hususani kifungu nilichokinukuu hapo juu, na Maandiko yale kabla yake (Shemot 19:1–19:6) na pia Maandiko yanayofuatia, ambayo ni Asereti D’broti (Maneno / Amri Kumi). Kufuatana na mtazamo wako, ni tukio la namna gani tunaelezewa kupitia Maandiko haya?

Tukio katika visehemu hivi vinaelezea Neno la M-ngu likienenda toka kwa M-ngu kwenda kwa taifa lililoagizwa kulieneza ulimwenguni. Kwa hiyo Parasha yetu ya wiki hii inaelezea tukio linalofanana na yale yaliyoelezewa katika visehemu vya Vitabu vya Yekhezikieli na Hitigaluti, ambavyo kama tujuavyo, vyote vinaelezea nyakati ambapo Neno la M-ngu litaenenda toka kwa Mungu na kwenda ulimwengu kote kuisikia na kuipokea Torati ya M-ngu. Matukio yote yaliyoelezewa pote katika Yekhezikieli na Hitigaluti bado hayajatokea. Kwa hiyo tukio la Hari Sinai katika Parasha yetu ni namna ya matukio haya ambayo yatakuja kutokea.

Enjoyed this Post? Subscribe to our RSS Feed, Follow us on Twitter, make a Comment or simply recommend us to friends and colleagues!

Tzedakah

More Related Articles:


Leave a Reply

Parashat Beha'alotcha
Torah Portion: Numbers 8:1-12:16


  1. Bamidbar 8:1-14 (Sunday)
  2. Bamidbar 8:15-26 (Monday)
  3. Bamidbar 9:1-14 (Tuesday)
  4. Bamidbar 9:15-10:10 (Wednesday)
  5. Bamidbar 10:11-34 (Thursday)
  6. Bamidbar 10:35-11:29 (Friday)
  7. Bamidbar 11:30-12:16 (Saturday)

Haftarah / Prophets

  • Zechariah 2:14 - 4:7 (Saturday)

Besorah / Good News

  • 1 Corinthians 10:6-13 (Saturday)
Radio Mashiach
Sifrei Chaim - Messianic Jewish Judaica
Tzedakah
Find out on Facebook

Important Links

Special links

  • Offering New Alternatives to Homosexuality
Contact us

A Torah centred Messianic Jewish יהודים משיחים kehila, Toronto, Ontario, Canada - An ever changing Messianic Jewish website till King Mashiach Yeshua comes back!!!
אנחנו רוצים משיח עכשיו / Мы хотим Машиаха сейчас / We Want Mashiach Now / Queremos al Mashiaj ya - יחי אדוננו מורנו ורבינו מלך המשיח לעולם ועד